FAQ

Search our FAQs below

FAQs

Je, data iliyo kwenye dodoso hili itatumikaje?
Baada ya kujisajili, kwa nini nilipokea ujumbe kutoka anwani za barua pepe (vikoa) tofauti na NHK WORLD-JAPAN?
Je, kwa nini nilipokea mialiko ya kushiriki katika tafiti ambazo hazihusiani na NHK WORLD-JAPAN?
Wakati mwingine utaombwa kushiriki katika tafiti kutoka kampuni nyingine tofauti na NHK WORLD-JAPAN. Matokeo yatatumika kutangaza na kukuza shughuli za kampuni hizo, na vile vile yataonekana katika bidhaa na huduma mpya. Tutashukuru sana kwa ushirikiano wako
Je, naweza kuthibitisha salio la alama zangu?
Je, ninaweza kubadilisha pointi nilizokusanya nipewe kitu gani?
Ninaweza kuangalia maudhui ya maelezo niliyosajili wapi?
Data yangu iliyosajiliwa inadhibitiwa kwa usahihi?
Je, nifanyeje iwapo sitaki tena kushiriki kama mwanajopo?
Je, nitapokea barua zozote za kunishawishi ninunue chochote?
Je, maelezo ya kibinafsi yanashughulikiwaje?

Kwa pamoja, data ambayo haimtambulishi mtu yeyote binafsi iliyo kwenye tafiti itatumika na NHK WORLD-JAPAN ili kuboresha maudhui yao. Tafiti kutoka makampuni mengine tofauti na NHK WORLD-JAPAN zitatumika kwa ajili ya shughuli za kutangaza na kukuza kampuni hizo, pamoja na kuonekana katika bidhaa na huduma mpya.

Udhibiti wa data yako iliyosajiliwa, pamoja na udhibiti wa jopo la utafiti unafanywa na shirika la kukusanya data na teknolojia la nchini Litwania linaloitwa Syno International. Barua pepe za usajili na uthibitisho zitatumwa kutoka info@synopanel.com Kwa maelezo zaidi kuhusu Syno International, tafadhali bofya hapa.

Wakati mwingine utaombwa kushiriki katika tafiti kutoka kampuni nyingine tofauti na NHK WORLD-JAPAN. Matokeo yatatumika kutangaza na kukuza shughuli za kampuni hizo, na vile vile yataonekana katika bidhaa na huduma mpya. Tutashukuru sana kwa ushirikiano wako

Haina gharama. Usajili na huduma haina gharama yoyote.

Ingia tu katika akaunti yako, utaona salio lako katika kona ya juu upande wa kulia. Ukibofya kichupo, utatumia pointi zako na pia utaweza kuona historia yako ya zawadi ulizojizolea. Kiwango cha chini kinalingana na Euro 10.

Ukishakusanya alama za chini zinazoruhusiwa kujipatia zawadi, unaweza kubadilisha kiasi hicho cha pesa upewe pesa taslimu au kadi ya zawadi. Tafadhali rejelea hapa ili upate maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kubadilisha pointi zako katika nchi unakoishi.

Ukiingia katika akaunti yako, utapata kichupo cha Mtumiaji kwenye kona ya juu upande wa kulia.

Data yako iliyosajiliwa inadhibitiwa kwa umakini mkubwa na Syno International, Inc. Ili uangalie sera yake ya faragha, bofya hapa. .

Ingia katika akaunti yako na ubofye kichupo cha Mtumiaji. Bofya “Badilisha akaunti”. Katika sehemu ya chini utaona ujumbe unaoitwa “Jiondoe kwenye JOPO”. Bofya ujumbe huo.

Kwa kushiriki katika utafiti huu, hutapokea barua zozote zinazokushawishi ununue chochote kutoka kwa kampuni zinazohusika.

Data yote ya binafsi unayotoa hudhibitiwa kwa umakini mkubwa na Syno International, Inc. kwa mujibu wa Sera yake ya Faragha. Ikiwa unataka kupata maelezo zaidi tafadhali rejelea hati zetu za sera ya faragha hapa.

Data yako ya binafsi inaweza kupeanwa kwa madhumuni ya kutumiwa na Jopo la Utafiti la NHK WORLD_JAPAN na kuendesha tafiti katika mashirika yafuatayo: NHK, NHK International Inc., na Kituo cha Utafiti cha Nippon. Wadau wote wanaohusika wanajitolea kulinda data yako ya binafsi kwa mujibu wa sheria inayotumika.